Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

DRC: Mahakama ya katiba yaidhinisha ushindi wa Tshisekedi

Mahakama ya katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC imetoa uamuzi katika kesi iliyowasilishwa na kinara wa upinzani Martin Fayulu, ambapo imetupilia mbali pungamizi lake na kuidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi.

Majaji wa mahakama ya katiba nchini DRC wakisikiliza kesi ya Martin Fayulu, jumanne January 15 2019.
Majaji wa mahakama ya katiba nchini DRC wakisikiliza kesi ya Martin Fayulu, jumanne January 15 2019. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo wa mahakama unamaanisha kuwa sasa Tshisekedi anaweza kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ifikapo january 22, Jumanne ya wiki ijayo.

Katika hatua nyingine mgombea wa upinzani wa Lamuka Martin Fayulu, yeye ameitaka jumuia ya kimataifa kutomtambua Bwana Tshisekedi kuwa rais wa DRC, kufwatia kile alichosema kuwa chama cha upinzani cha UDPS pamoja na chama tawala wameiba kura za wananchi.

Fayulu anadai kwamba Felix Tshisekedi na Rais Joseph Kabila walifanya mpango wa siri na kukubaliana faraghani, baada ya matokeo ya awali kuonesha kwamba mgombea ambaye alikuwa akiungwa mkono na Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary, ameshika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake msemaji wa rais Mteule Tshisekedi na mshauri katika masuala ya kisiasa, Thotho Mabiku, ametowa kwa Martin Fayulu wakuungana na kiongozi huyo, akisema ni fursa kwa wanasiasa wote DRC kuchangia ujenzi wa taifa hilo kubwa

Punde baada ya mahakama kutoa uamuzi huo Bi Eve Bazaiba ambaye ni msemaji wa muungano wa upinzani wa Lamuka amewataka wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi huo

Haya yanajiri wakati mwandishi wetu wa Kinshasa Freddy Tendilonge akithibitisha kuwa huduma ya mtandao wa Intaneti imerejea tena usiku wa kuamkia hii leo baada ya kufungwa kwa muda wa siku kadhaa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.