Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-UBELGIJI-GBAGBO-ICC-MARIDHIANO

Ubelgiji: Tuko tayari kumpokea Gbagbo ikiwa ataachiliwa huru

Ubelgiji imesema iko tayari kumpokea kwenye ardhi yake aliyekuwa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo aliyefutiwa mashitaka hivi karibuni na Mahakama ya Kimataifa ya Ihalifu (ICC) na kuamuru aachiliwe huru.

Laurent Gbagbo na mwanasheria wake Emmanuel Altit katika ufunguzi wa kesi yake Januari 28,2016.
Laurent Gbagbo na mwanasheria wake Emmanuel Altit katika ufunguzi wa kesi yake Januari 28,2016. REUTERS/Peter Dejong/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Mwendesha mashitaka wa ICC Fatou Bensouda hivi majuzi alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuachiliwa huru siku moja baada ya ICC kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru.

Katika mahojiano maalum na RFI Idhaa ya kifaransa, waziri Mamadou Toure anayehusika na Vijana pia Naibu Msemaji wa chama cha RHDP, amefahamisha Serikali ya Ubelgiji imesema iko tayari kumpokea Gbagbo lakini haitakubali kumpokea Ble Goude.

“Laurent Gbagbo ni mwanasiasa na ambacho tunafahamu ni kwamba atakuwa huko Ubelgiji. Serikali ya ubelgiji na yenyewe imethibitisha dhahiri kuwa itampokea atakwenda ubelgiji. Sasa hatua ya Laurent Gbagbo kurejea Cote d'Ivoire ni jambo ambalo litajadiliwa kwa undani kati ya Laurent Gbagbo na Rais Allassan Ouattara. kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo Ubelgiji imekataa kumpokea Charles Ble Goude”, amesema Mamadou Toure.

Katika hatua nyingine Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda, ameomba Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude kuendelea kuzuiliwa jela, wakati anaendelea kupata na kutathmini sababu zilizopelekea majaji kuamua kuachiliwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.