Pata taarifa kuu
DRC-YUMBI-MAUAJI-USALAMA

Mauaji ya Yumbi DRC yazua maswali mbalimbali na kuushangaza ulimwengu

Watu zaidi ya 890 waliouawa kwa muda wa siku mbili mnamo mwezi Desemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, idadi ambayo inaonyesha hali ya kutisha lakini idadi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo iliyotangazwa, kwa mujibu wa mashirika ya kiraia.

Yumbi inapatikana katika eneo la Mai-Ndombe, DRC.
Yumbi inapatikana katika eneo la Mai-Ndombe, DRC. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ambayo inasema watu hao waliuawa katika mapigano ya kikabila kati ya tarehe 16 na 18 Desemba katika vijiji vinne vya eneo la Yumbi, magharibi mwa DRC.

Idadi hiyo ni ndogo kwa sababu wengi wa waliouawa walitupwa katika mto au kuchomwa moto, imesem atume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Na hivyo ndivyo wanavyofikira wakaazi wa eneo hilo lililokumbwa na machafuko mabaya, wakiomba wahusika wafikishwe wafahamike na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Waziri wa Habari na msemaji wa serikali ya DRC, amesema hawezi kuthibitisha ukweli wa idadi hiyo ya watu lakini akasema, serikali inafahamu watu waliopoteza maisha ni 100.

Mzozo kati ya makabila ya Banunu na Batende ulizuka baada wakuu wa kabila la Banunu kuamua kumzika mmoja wa viongozi wao katika ardhi ya kabila la Batende.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.