Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Uchaguzi DRC: Umoja wa Afrika wawalika majirani wa DRC Addis Ababa

media Afisa wa CENI akihesabu kura, Kinshasa, Januari 4 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Baz Ratner

Viongozi wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanakutana Alhamisi wiki hii kwa dharura katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwa ombi la Rais wa Umoja wa Afrika Paul Kagame, ili kujadili hali inayoendelea nchini DRC.

Lengo la mkutano huo ni kujadili matokeo ya uchaguzi wa urais wa Desemba 30 yanayoendelea kuzua utata nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Njia za kuondokana na mgogoro huo ni tatu tu: Aidha kuhesabu upya kura, kukutana kwa mazungumzo na wanasiasa nchini DRC au kukubali matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi (CENI). Nchi jirani za DRC zinatarajia kutafutia suluhu mgogoro huu. Viongozi kumi na wanne wa nchi za ukanda huo wamealikwa kushirika katika kikao cha Umoja wa Afrika kwa ombi la Rais wa Umoja wa Afrika Paul Kagame.

Mwishoni mwa wiki iliyopita SADC iliomba kura zirudi tena kuhesabiwa upya, saa chache baadae jumuiya hiyo ilibadili kauli kwa shinikizo la Afrika Kusini, mshirika wa serikali ya Kinshasa na kusema kwamba wanaheshimu uhuru wa DRC.

Lengo la mkutano wa Addis Ababa ni kutoa kauli moja. Kuanzia Alhamisi asubuhi, kuna mazungumzo ambayo yanafanyika kati ya Rais Paul Kagame, viongozi wa nchi za SADC na zile za ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).

"Si rahisi wakati matokeo ya uchaguzi yanapingwa," RAis Paul Kagame amesema.

Kwa kweli ikiwa asilimia 61 ya Wakongo walipigia kura Martin Fayulu, kama anavyodai mgombea, kumyima ushindi wake kuna hatari ya kuzuka machafuko nchini, wanasema wadadisi.

Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani wakuu walioshindwa katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018, ameendelea kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi yanayompa ushindi Felix Tshisekedi Tshilombo, kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS, ambaye alishinda kwa 38.57% ya kura.

Mahakama ya Katiba inaendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais iliyofunguliwa na Martin Fayulu.

Matokeo hayo pia yanapingwa na mgombea mwingine, Theodore Ngoyi, ambayae anataka uchaguzi huo ufutwe mara moja.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana