Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-ICC-MARIDHIANO

Serikali ya Cote d'Ivoire yataka wananchi kuboresha maridhiano

Serikali ya Cote d'Ivoire imewatolea wito wananchi kuboresha maridhiano na kushikamana kwa hali na mali. Kauli hii inakuja baada ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuchukua uamuzi wa kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru.

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara.
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Gbagbo bado anakabiliwa na kifungo cha miaka 20, hukumu iliyochukuliwa na mahakama nchini Cote d'Ivoire mnamo mwezi Januari 2018 kwa uhalifu wa kiuchumi.

Licha ya hukumu hiyo, hakuna uwezekano wowote kwamba polisi ya Cote d'Ivoire itajaribu kumzuia ikiwa atarudi nchini.

"Uamuzi wa kurudi" nchini Cote d'Ivoire "ni wake", serikali ya Cote d'Ivoire ilitangaza siku ya Jumatano saa chache baada ya kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo "kuwa watulivu, kusameheana na kuboresha maridhiano."

Laurent Gbagbo ambaye yuko kizuizini kwa miaka saba sasa kwa uhalifu uliotekelezwa wakati wa machafuko yaliyotokea mwaka 2010-2011, yaliyotokana na kukataa kwake kukabidhi madaraka kwa mpinzani wake , Rais wa sasa wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara.

Hatimaye alikamatwa mwezi Aprili 2011 na vikosi vya Rais Ouattara, vikisaidiwa na Umoja wa Mataifa na Ufaransa. Laurent Gbagbo ni rais wa zamani wa kwanza kufikiswa mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Waathirika wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2011 nchini Côte d'Ivoire wakiandamana jijini Abidjan Januari 14, 2019.
Waathirika wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2011 nchini Côte d'Ivoire wakiandamana jijini Abidjan Januari 14, 2019. Sia KAMBOU / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.