Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu 11 wauawa katika machafuko DRC

media Polisi karibu na makao makuu ya CENI mjini Kinshasa, Januari 10. © REUTERS/Baz Ratner

Saa chache baada ya Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI )kumtangaza Felix Tshisekedi Tshilombo mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo, baadhi ya maeneo yalikumbwa na machafuko, ambayo yamesababisha watu 11 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.

Watu sita wamepoteza maisha katika mji wa Kikwit, katika mkoa wa Kwilu, mashariki mwa mji wa Kinshasa, na wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa mashahidi.

Ripoti zinasema waliopoteza maisha ni maafisa wawili wa polisi, kwa mujibu wa chanzo cha polisi.

Maafisa wawili wa polisi na raia wanne ndio waliopoteza maisha katika makabiliano ya kupinga matokeo hayo, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka Kikwit.

Katika mji wa Kimbanseke watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 22 kujeruhiwa wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa Martin Fayulu na wale wa Felix Tshisekedi.

Katika miji kadhaa ya nchi hiyo kulishuhudiwa maandamano ya furaha na makabiliano kati ya vikosi vya usalama na watu weny hasira wakipinga matokeo hayo ya uchaguzi

Watu wengine 10 wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.

Mapema Alhamisi wiki hii Umoja wa Afrika kupitia msemaji wake uliwatolewa wito wananchi wa DRC kuwa na utulivu na kuwataka wagombea ambao hawakuridhishwa na matokeo hayo kutumia utaratibu wa sheria kwa amani kwa kuwasilisha madai yao mbele ya Mahakama ya Katiba.

Hayo yanajiri wakati ambapo leo Ijumaa kunasubiri kutangazwa washindi katika uchaguzi wa wabunge na magavana wa mikoa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana