Pata taarifa kuu
DRC-LAMUKA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais DRC: Kambi ya Martin Fayulu yadai imepata ushindi kwa asilimia 61 ya kura

Martin Fayulu, mgombea wa upinzani, ambaye alichukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, ametangaza kuwa atawasilisha malalamiko yake mahakamani siku ya Jumamosi dhidi ya ushindi wa Felix Tshisekedi katika Mahakama ya Katiba.

Le candidat à l'élection présidentielle Martin Fayulu, fait signe à ses partisans à son arrivée à l'aéroport international de N'djili à Kinshasa, en République démocratique du Congo, le 21 novembre 2018.
Le candidat à l'élection présidentielle Martin Fayulu, fait signe à ses partisans à son arrivée à l'aéroport international de N'djili à Kinshasa, en République démocratique du Congo, le 21 novembre 2018. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa muungano wa upinzani Lamuka Fayulu ameshinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 61 ya kura dhidi ya 18% alizopata Felix Tshisekedi.

Muungano wa upinzani Lamuka umetangaza leo Ijumaa kura ambazo mgombea wake Martin Fayulu alipata katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30.

Kwa mujibu wa Lamuka, ikinukuu twikimu zilizotolewa na maafisa wake 220,000 walitumwa katika vituo mbalimbali wakati wa Uchaguzi Mkuu nchini DRC, Fayulu alipata 61% ya kura na Félix Tshisekedi alipata 18% ya kura.

Takwimu hizi zilitolewa na Fidèle Babala, mmoja wa makada wa Lamuka, mbele ya mamia ya wafuasi wa muungano Lamuka katika makao makuu ya chama cha MLC, mjini Kinshasa.

Babala ametangaza matokeo ya uchaguzi mkoa kwa mkoa. Fayulu, ambaye amekuepo katika mkutano huo amelaani matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (CENI) ambayo yanampa ushindi Felix Tshisekedi Shilombo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.