Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Fayulu; Tuko tayari kuwasilisha malalamiko yetu mahakamani

Mgombea wa uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano wa upinzani Lamuka, Martin Fayulu, ambaye alichukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30 nchini DRC anatarajia kuwasilisha malalamiko yake mahakamani.

Mgombea wa uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano wa upinzani Lamuka, Martin Fayulu, Novemba 21, 2018.
Mgombea wa uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano wa upinzani Lamuka, Martin Fayulu, Novemba 21, 2018. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

"Tuko tayari kuwasilisha malalamiko yetu ya kuibiwa kura katika Mahakama ya Katiba", amesema Bw Fayulu.

Timu yake ya kampeni inasema ilikusanya 61.51% ya kura alizopata mgombea Fayulu, dhidi ya % 18.86 tu alizopata mshindi aliyetangazwa Felix Tshisekedi Tshilombo, mgombea mwengine wa upinzani, aliyepeperusha bendera ya chama cha UDPS - ambaye Tume ya Uchaguzi (CENI) inasema alipata 38.57% ya kura.

Mgombea anayeungwa mkono na rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Emmanuel Ramazani Shadary, aliyechukuwa nafasi ya tatu alipata 18.49% ya kura, amesema Fidele Babala, afisa wa kampeni ya Fayulu.

"Tunajua kwamba Mahakama ya Katiba inaundwa na wafuasi wa Joseph Kabila lakini hatutataki waje waseme kuwa hatukufuata sheria. Tunataka kufanya tunachokiweza ili kupata matokeo ya haki na ya wazi, "Martin Fayulu ameiambia BBC.

Katika mahojiano na Radio France Internationale (RFI) siku ya Alhamisi, Fayulu, ambaye alionekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi kulingana na uchunguzi ulioendeshwa kabla ya uchaguzi huo, tayari amelaani kile alichokiita "mapinduzi ya uchaguzi" na "matokeo ambayo hayafanani na ukweli wa uchaguzi."

Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa saa tisa usiku wa kuamkia Alhamisi wiki hii na Tume ya Uchaguzi (CENI). Kuanzia wakati tangazo hilo lilipotolewa, Martin Fayulu ana saa arobaini na nane kuwasilisha malalamiko yake mahakamani dhidi ya matokeo hayo ya uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.