Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

AU yataka mvutano kuhusu matokeo ya urais nchini DRC kutatuliwa kwa amani

media Tume ya Uchaguzi CENI ikitangaza matokeo ya uchaguzi wa urais, Kinshasa, tarehe 10 Januari 2019. REUTERS/Jackson Njehia

Mkuu wa Tume ya Umoja hiyo Moussa Faki Mahamat amesema kama kuna dukudkuku kuwa, matokeo hayo sio sahihi, mazungumzo ya kisiasa pia yatumiwe kutatua mzozo wowote.

Tume ya Uchaguzi CENI ilimtangaza Felix Tshisekedi kama mshindi wa uchaguzi wa urais nchini DRC, matokeo ambayo yamepingwa vikali na Martin Fayulu kutoka muungano wa upinzani ambaye amesema kutangazwa kwa Tshisekedi kama mshindi ni mapinduzi ya uchaguzi.

Ufaransa kupitia kwa Waziri wa Mambo ya nje Jean Vyes Le Drian, amesema matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na CENI hayakuwa sahihi.

Mataifa mengine kama Ubelgiji, Uingereza yametilia shaka matokeo hayo.

Nalo Baraza la Maaskofu nchini humo limesema matokeo yaliyotangazwa hayaendani na matokeo waliyokusanya kutoka kwa waangalizi wao.

Hata hivyo, wametoa wito kwa wale wanaopinga matokeo hayo kutumia njia za kisheria kuyapinga.

Mahakama ya Katiba ina wiki moja kupitia matokeo hayo na kuyathibitisha au kuyakataa kabla ya rais mpya hajaapishwa.

Kufuatia mvutano huo unaoendelea nchini DRC, baadhi ya miji nchini DRC ilikumbwa na machafuko jana Alhamisi.

Kwa mujibu wa mashahidi watu 11 wameuawa katika machafuko hayo.

Watu sita ikiwa ni pamoja na polisi wawili waliuawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa Martin Fayulu na vikosi vya usalama katika mji wa Kikewit ambayo ni ngome ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu.

Machafuko hayo pia yameshuhudiwa katika miji ya Kisangani, Kananga, Kasaï, Tshikapa, Kimbanseke, Ngaba na Lemba.

Kwa ujumla watu 11 wameuawa katika machafuko nchini DRC kwa siku tu ya Alhamisi, kwa mujibu wa mashahidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana