Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI-USALAMA

Jeshi la Marekani laendelea na mashambulizi yake Somalia

Vikosi vya Marekani vinaendelea na mashambulizi yake ya angani nchini Somalia dhidi ya wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab.

Jeshi la Marekani lilisema kuwa liliendesha mashambulizi dhidi ya Al Shabab katika eneo la Harardhere kilomita zaidi ya mia moja kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu Oktoba 12, 2018.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa liliendesha mashambulizi dhidi ya Al Shabab katika eneo la Harardhere kilomita zaidi ya mia moja kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu Oktoba 12, 2018. GOOGLE MAPS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili vikosi vya Marekani viliendesha mashambulizi ya angani dhidi ya kambi ya wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab karibu na mji wa Yaaq Braawe, kusini magharibi mwa Somalia, na kuua wapiganaji sita na kuharibu gari moja, uongozi wa jeshi la Marekani katika kanda ya Afrika (Africom)   taarifa yake.

Hili ni shambulizi la tatu la Marekani dhidi ya wapiganaji wa Al Shabab ndani ya siku tatu. Siku ya Jumanne jeshi la Marekani lilisema kuwa liliua siku moja kabla wapiganaji wanne wa Al Shabab karibu na mji wa Baqdaad, sio mbali na mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, na shambulizi jingine karibu na mji wa Dheerow Sanle, kusini Magharibi mwa Somalia liliua wapiganaji sita wa Al Shabab siku ya Jumapili.

Januari 3 jeshi la Marekani lilibaini kwamba liliua wapiganaji kumi wa Al Shabab Januari 2 karibu na mji wa Dheerow Sanle.

Katika kila tangazo, jeshi la Marekani linabaini kwamba lengo la Marekani na washirika wake - serikali ya Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) - ni kuzuia Al Shabab kupiga kambi katika maeneo ambapo wanaweza kupata urahisi wa kukukimbilia kwa "kuandaa na kuendesha mashambulizi ya kigaidi, kuiba misaada ya kibinadamu, kujipatia fedha kiurahisi kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, fedha ambazo zitafadhili shughuli zake na kuwapa hifadhi magaidi."

Jeshi la Marekani "litaendelea kushirikiana na washirika wake katika kukabidhi serikali ya Somalia jukumu la muda mrefu la kusimamia usalama wa Somalia kutoka AMISOM," Africom imesema katika taarifa yake Jumatano wiki hii.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kituo cha habari cha Marekani cha NBC, Trump aliitaka Pentagon kupunguza kwa kiasi kikubwa shughuli za kijeshi nchini Somalia.

Trump aliamua mwezi Desemba kuwaondoa askari wote wa Marekani nchini Syria na pia kutathmini kuanza kupunguza askari wake nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.