Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
Afrika

Felix Tshisekedi atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais DRC

media Felix Tshisekedi Tshilombo ashinda uchaguzi wa rais DRC. © REUTERS/Baz Ratner/File Photo

Tume ya Uchaguzi hatimaye imetangaza matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 mwaka jana nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo. Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi Tshilombo ndiye aliibuka mshindi katika uchaguzi huo akipata asilimia 38.57 ya kura, kwa mujibu wa CENI.

Ushindi huo uliotangazwa na CENI ni wa kihistoria kwa chama cha UDPS na Tshisekedi mwenyewe.

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni (sawa na asilimi 34), huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni(sawana na asilimia 23).

Matokeo kamili yanatarajiwa kutangazwa Januari 15 na rais mpya ataapishwa siku tatu baadaye, kulinagana na ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI).

Felix Tshisekedi, ni mwanawe mwanzilishi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu Etienne Tshisekedi.

Babake alifariki Februari mwaka jana na sasa mwanawe anatarajia kutumia msingi wa umaarufu wa babake kuchaguliwa kuwa rais.

Marafiki zake humuita kwa jina la utani "Fatshi" kutokana na hali kwamba yeye ni mnene kiasi.

Kwa muda ilionekana kana kwamba Tshishekedi, 55, jina lake halingekuwa kwenye karatasi za kura.

Iwapo matokeo hayo yatathibitishwa, Tshisekedi atakuwa rais naye Kamerhe, ambaye ni rais wa zamani wa Bunge na ambaye aliwania dhidi ya Kabila mwaka 2011 awe waziri mkuu.

Bw Tshisekedi atakuwa mgombea wa kwanza kabisa wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.

DRC, nchi kubwa ya Afrika ya kati ina utajiri wa madini na ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya cobalt, yanayotumiwa kwa simu na betri za magari.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana