Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika
DRC

Uchaguzi DRC: Fayulu aonya Tume ya Uchaguzi

media Martin Fayulu apiga kura katika mji wa Kinshasa, DRC, Desemba 30, 2018. © REUTERS

Mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais nchini DRC Martin Fayulu amesema kuwa wananchi wa DR Congo wanamfahamu "mshindi halisi wa uchaguzi wa urais", huku akionya Tume ya Uchaguzi (CENI) "dhidi ya jaribio lolote la kuficha ukweli wa matokeo ya uchaguzi".

Wananchi wa DRC tayari wanafahamu matokeo ya uchaguzi na wanamfahamu "mshindi halisi wa uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018," amesema Fayulu, katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari tangu uchaguzi wa Desemba 30.

Fayulu na wagombea wengine watano wameonya Tume ya Uchaguzi "dhidi ya jaribio lolote la kuficha ukweli wa matokeo ya uchaguzi".

Wametoa wito kwa Tume ya Uchaguzi "kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais haraka iwezekanavyo".

Tume ya Uchaguzi iliahirisha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, ikidai kuwa imekwisha hesabu tu asilimia 53 ya kura zilizopigwa.

Bw Fayulu amesema kuwa "CENI, baada ya kupata matokeo ya kweli ... ilijizuia kwa makusudi kutangaza matokeo hayo kwa kukiuka ratiba yake kwa sababu zisizoeleweka".

Hali hii inasababisha mvutano wa kisiasa, " ameongeza Bw Fayulu.

Siku ya Jumanne, chama cha kihistoria cha upinzani cha UDPS kilisema kuwa mgombea wake Felix Tshisekedi Tshilombo alishinda uchaguzi wa urais" na kwamba kuna haja ya mgombea wake na Rais Joseph Kabila kukutana na "kuandaa zoezi la kukabidhiana madaraka kwa amani.

Wagombea wakuu upande wa upinzani ni Martin Fayulu na Felix Tshisekedi Tshilombo, na upande wa muungano wa vyama vinavyoshiriki katika serikali viliwakilishwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Emmanuel Ramazani Shadary.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana