Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Askari waliojaribu kufanya mapinduzi ya kijeshi wakamatwa Gabon

media Vikosi vya usalama vya Gabon vikipiga doria katika maeneo jirani na makao makuu ya Radio na Televisheni ya taifa, ambapo kundi la wanajeshi walivamia wakijaribu kuipindua serikali, Januari 7, 2018. © Steve JORDAN / AFP

Vyombo vya usalama nchini Gabon vimefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi la hapo jana ambapo kiongozi wa wanajeshi walioshiriki jaribio hilo amekamatwa na wengine wawili wameuawa.

Jaribio hili limekashifiwa vikali na viongozi wa umoja wa Afrika, umoja wa Ulaya na umoja wa Mataifa ambao wamesema hakuna demokrasia itakayopatikana kwa nguvu ya kijeshi au kupitia mapinduzi.

Hali ya utulivu imerejea nchini humo huku usalama ukiwa umeimarishwa kwenye maeneo mengi ya nchi kwa mujibu wa msemaji wa Serikali ya Gabon, Guy Betrand Mapangou.

Balozi wa Gabon nchini Ufaransa, Flavien Enongoue, amesema uchunguzi tayari umeanza kubaini wanajeshi zaidi waliohusika.

Kwa upande wa msemaji wa kinara wa upinzani nchini humo Jean Ping, Laurence Ndong, amesema wao wameelewa kwanini wanajeshi hao walijaribu kuipindua Serikali.

Jaribio hili limefanyika wakati huu Rais Ali Bongo akiwa nchini Moroco ambako anapatiwa matibabu kwa zaidi ya miezi miwili sasa tangu aanze kuugua akiwa nchini Saudi Arabia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana