Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-USALAMA

Milio ya risasi yasikika katika mji mkuu wa Gabon

Sintofahamu imejitokeza nchini Gabon baada ya jeshi kutangaza kwenye radio ya taifa kuundwa kwa "Baraza la mpito la taifa". Tangazo hilo limetolewa usiku wa kuamkia Jumatatu hii Januari 7, 2019 na kundi la askari waliovamia radio ya taifa.

Gari la vikosi vya usalama vya Gabon likiegeshwa mbele ya makao makuu ya radio na televisheni ya taifa mjini Libreville, Juni 2017 (picha ya kumbukumbu).
Gari la vikosi vya usalama vya Gabon likiegeshwa mbele ya makao makuu ya radio na televisheni ya taifa mjini Libreville, Juni 2017 (picha ya kumbukumbu). © STEVE JORDAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo linaloongozwa na afisa wa cheo cha Luteni kutoka kikosi cha ulinzi wa rais Ondo Obiang Kelly, limetangaza kwamba baraza hilo la "mpito" litaundwa katika saa zijazo.

Katika tangazo hilo, jeshi linasema walipigwa na butwaa baada ya hotuba ya taifa ya tarehe 31 Desemba ya Rais wa Jamhuri Ali Bongo. "hotuba iliyozua mkanganyiko na utata" askari hao wamesema.

Askari waliovamia radio ya taifa mapema asubuhi wametangaza kwamba katika saa chache zijazo wataaunda "Baraza la mpito la taifa".

Kufuatia hali hiyo, baadhi ya viongozi wametakiwa kwenda kwenye makao makuu ya Bunge la taifa ikiwa ni pamoja na afisa wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais, Jenerali Ntumpa Lebani (aliyefungwa mwaka 2009 wakati Bongo alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi) na rais wa sasa wa Baraza la Seneti

Wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wajumbe wa vyama vya wafanyakazi na hata viongozi wa kidini pia ni miongoni mwa viongozi ambao wametakiwa kushiriki mkutano huo.

Kundi hilo la askari wamewataka askari wenzao kuchukua udhibiti wa njia za usafiri, ghala za silaha na vifaa vya jeshi, viwanja vya ndege na "kulinda taifa".

Wakati huo huo milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa nchi hiyo Libreville.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.