Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SANAA-SIASA

Zuma akumbwa na mzozo mwengine wa kisaia kufuatia albamu yake ya muziki

Rais wa zamani wa Afrika Kusini ametangaza kuanza kwa kazi yake mpya katika muziki. Kazi hii itaanza mwezi Aprili kwa nyimbo za kupigania uhuru wa Afrika Kusini.

Jacob Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa yanayohusishwa na mpango wa kununua silaha mwaka 1990.
Jacob Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa yanayohusishwa na mpango wa kununua silaha mwaka 1990. ©REUTERS/Siphiwe Sibeko/
Matangazo ya kibiashara

acob Zuma, mwenye umri wa miaka 76 amesaini mkataba na manispaa ya Durban, ambayo ilikubali kufadhili albamu ya nyimbo za kupigania uhuru zilizoimbwa na Zuma. Chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimesema mkataba huo una mashaka ndani yake.

Jacob Zuma aliimba nyimbo nyingi za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi wakati wa kazi yake ya kisiasa.

Katika kila mkutano wa ANC, mara nyingi alikuwa wa kwanza kuinuka, na kuanza kuimba nyimbo za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Nyimbo, ambazo zimemfanya kuwa maarufu nchini Afrika Kusini.

Jacob Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa yanayohusishwa na mpango wa kununua silaha mwaka 1990. Hata hivyo amekana makosa hayo.

Jimbo la Ethekwini lilikubali kufadhili albamu ya nyimbo za kupigania uhuru zilizoimbwa na Zuma, ambazo viongozi walisema zingehifadhi sehemu ya urithi wa kitamaduni.

Ethekwini inashirikisha mji wa pwani wa Durban na miji jirani ya Kwa Zulu-Natal, na jimbo la nyumbani kwa Zuma ambako ndiko kuna wafuasi wake wengi.

Kiongozi Zwakele Mncwango wa chama cha DA amesema kuwa rasilimali za serikali za eneo hilo zinatakiwa kutumika kusaidia vijana kujiajiri katika sekta ya muziki.

Wakati wa vita dhidi ya uongozi wa wakoloni waliokuwa wachache nchini Afrika Kusini, nyimbo zilitumika sana kuimarisha uungwaji mkono na kuimarisha motisha ya waandamanaji.

Baadhi ya raia wa Afrika Kusini anamuona Zuma kama mtu mwenye kipaji na anelewa historia ya muziki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.