Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Umoja wa Afrika: Uchaguzi ulikwenda vizuri DRC

Umoja wa Afrika (AU) umesema unatarajia kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa Jumapili nchini DRC yatatangazwa "kulingana na kura" iliyopigwa na Wakongo, Umoja huo umesema siku ya Jumatano wiki hii mjini Kinshasa.

Dioncounda Traoré (picha ya kumbukumbu).
Dioncounda Traoré (picha ya kumbukumbu). © AFP PHOTO /BERTRAND LANGLOIS
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika ulituma waangalizi 80 kufuatilia na kutathmini mchakato wa uchaguzi.

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika (MOEUA) "unatarajia sana kwamba matokeo yatakayotangazwa yataendana na kura iliyopigwa na wananchi wa DRC," amesema kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, rais wa zamani wa mpito wa Mali Dioncounda Traoré, katika taarifa yake ya awali ya uchunguzi.

Uchaguzi Mkuu wa Jumapili nchini DRC ulifanyika katika hali ya "utulivu na amani, licha ya kuingiliwa kati na changamoto zote za kisiasa na za usalama zilizojitokeza," AU imesema.

"Hata hivyo, Umoja wa Afrika unasema kwamba kufanyika kwa uchaguzi huu, ambao uliahirishwa mara tatu, "ni ushindi mkubwa wa kwanza kwa wananchi wa DRC".

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) pia umebainisha kuwa uchaguzi "ulifanyika katika mazingira na mchakato wa uchaguzi ulikwenda vizuri, na kuruhusu wananchi wengi wa DRC kutekeleza haki yao ya kupiga kura" .

Pamoja na waangalizi 73 katika mikoa 16 kati ya 26, SADC imebaini kwamba "59% ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati, licha ya kuwa baadhi vilichelewa kufunguliwa kwa muda wa dakika 45 hadi saa tano".

Uchaguzi ulifanyika kote DRC, ispokuwa katika maeneo ya Beni, Butembo (mashariki mwa DRC) na Yumbi (magharibi mwa nchi) ambako uchaguzi uliahirishwa kwa sababu za usalama na ugonjwa wa Ebola.

Tume ya Uchaguzi (CENI) imesema kwamba itatangaza matokeo ya awali ya uchaguzi kabla ya Jumapili, tarehe 6 Januari 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.