Pata taarifa kuu
MWAKA-MPYA-2019-DUNIA-AFRIKA

Dunia yaukaribisha mwaka mpya wa 2019 kwa shamrashamra

Raia wa mataifa mbalimbali barani Afrika na kwIngineko duniani wameupokea mwaka mpya wa 2019, kwa shangwe na kusherehekea kwa njia mbalimbali katika maeneo ya kuabudu, kumbi za starehe huku viongozi mbalimbali wakitoa ujumbe wao wa mwaka mpya. 

Mwaka mpya wa 2019
Mwaka mpya wa 2019 REUTERS/Pavel Rebrov
Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya, raia wa nchi hiyo walifurika katika maeneo mbalimbali kama makanisani na kumbi za starehe kuukaribisha mwaka mpya.

Jijini Nairobi, kulikuwa na tamasha kubwa ya muziki wa Injili katika uwanja wa jumba la mikutano ya Kimataifa, KICC ambapo maelfu walikesha kuusubiri mwaka mpya.

Katika hotuba yake ya mwaka mpya, rais Uhuru Kenyatta, ametoa wito kwa wakenya kuendeleza mshikamano wa kisiasa, ulioanza mwaka 2018, baada ya yeye na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuamua kusitisha uhasama wa kisiasa.

"Nawaomba tushirikiane sote, katika kuwaunganisha wananchi wetu, mshikamano tulioanza mwaka uliopita, umeleta manufaa makubwa," alisema rais Kenyatta.

Nchini Uganda, raia wa nchi hiyo nao pia walikesha katika maeneo mbalimbali, baada ya kumsikiliza rais wao Yoweri Museveni ambaye ameonya kuwa serikali yake haitamvulia yeyote atakayehusika katika visa anavyosema ni vya utovu wa nidhamu.

"Wazalendo wa nchi hii wameendelea kuhakikisha kuwa, nchi inakuwa dhabiti, hatutaruhusu yeyote atakaye kwenda kinyume na malengo yetu kwa kutekeleza uhalifu," alionya rais Museveni.

Sherehe za mwaka mpya
Sherehe za mwaka mpya PHOTO | PETER PARKS | AFP

Naye rais wa Tanzania John Magufuli katika ujumbe wake wa mwaka mpya, amewataka wananchi wa taifa hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika mwaka mpya.

“Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa
Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini, waachane na utamaduni wa
kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu, huo ni ugonjwa ambao
umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama
ni kwa mujibu wa sheria hawataki kujiamini, na wanasema hili ni maagizo
kutoka juu” amesema rais Magufuli.

Na huko nchini Rwanda rais Paul Kagame katika hotuba yake amewataka raia wa nchi yake  kuwa waangalifu licha ya kwamba nchi hiyo inaendelea kuwa salama.

Hata hivyo, ameyashtumu baadhi ya mataifa jirani ambayo yanaunga mkono makundi ya waasi ya FDRL na RDC.

Nchini Ufarasansa rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron amewataka wananchi wake kuwa wavumilivu wakati huu serikali yake ikiendelea kuboresha maendeleo yao.

Mwaka huu unapoanza amatarajio ni mengi kwa wananchi wa mataifa mbalimbali, hususan kule nchini DRC wananchi wanatarajia kumpata rais mpya.

Nchini Nigeria Uchaguzi utafanyika mwezi Februari.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.