Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DRC-JOSEPH KABILA-CENI

Zoezi la kupiga kura lamalizika, huku changamoto kadhaa zikiripotiwa

Zoezi la kupiga kura limemalizika katika maeneo mengi ya DRC huku changamoto kadhaa zikiripotiwa katika maeneo mbalimbali.

Rais Joseph Kabila akipiga kura Mjini Kinshasa leo Disemba 28 mwaka 2018
Rais Joseph Kabila akipiga kura Mjini Kinshasa leo Disemba 28 mwaka 2018 Baz Ratner/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za hivi punde kutoka kwa mwandishi wetu Sonia Rolley zinasema baadhi ya vituo vya kupigia kura katika eneo la Inongo vimechomwa moto.

Zaidi ya wapiga kura milioni 40 walijiandikisha katika daftari la kupigia kura lakini idadi ya waliojitokeza huenda ikawa pungufu. Hata hivyo bado ripoti kutoka maeneo mbalimbali ya taifa hilo hazijabainisha kwa kina namna zoezi la upigaji kura lilivyoendeshwa.

Mapema leo mvua ilitatiza shughuli za upigaji kura katika Jiji la Kinshasa.

Rais Joseph Kabila sanjari na mgombea wa muungano wa chama tawala FCC, Ramazan Shadary walipiga kura katika Jiji la Kinshasa, pia mgombea wa muungano wa Lamuka Martin Fayulu alipiga kura Mjini Kinshasa.

Tume ya uchaguzi inatazamiwa kuanza zoezi la kuhesabu kura lakini mshindi wa kiti cha urais atatangazwa Januari 15 na kuapishwa Januari 18.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.