Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Uchaguzi DRC: Vituo kadhaa vya kupigia kura vyachomwa moto Inongo

Uchaguzi Mkuu nchini DRC ambao umefanyika katika maeneo mbalimbali nchini humo umeingiliwa na dosari, huku mashrika mbalimbali yakikosoa namna uchaguzi huo ulivyoandaliwa.

Mwanamke huyu akipiga kura katika kituo cha kupigia kura mjini Kinshasa Desemba 30, 2018.
Mwanamke huyu akipiga kura katika kituo cha kupigia kura mjini Kinshasa Desemba 30, 2018. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya vituo vya kupigia kura vimefungwa huku, vingine vikichomnwa moto kwa tuhuma za udanganyifu.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa habari Sonia Rolley, katika eneo la Inongo, vituo viwili vya kupigia kura ndivyo vimefanya kazi, vingine vimechomwa moto baada ya tuhuma za udanganyifu.

Wakati huo huo Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco), katika taarifa yake, limebaini kwamba jumla ya vituo vya kupigia kura 12 300 walivyoorodhesha (56%): vituo vya kupigia kura 846 vimewekwa katika maeneo yaliyokatazwa. Ripoti 1,543 za matukio mabaya ikiwa ni pamoja na kesi 544 za matatizo ya mashine za kupigia kura, kesi 115 za wawakilishi mbalimbali kukataliwa kuingia katika vituo vya kupigia kura, kesi 86 za kufukuzwa kwa mashahidi, kesi 44 za rushwa, kesi 194 za vifaa kuharibiwa.

Mapema mchana wakaazi wa Beni moja ya maeneo ambayo uchaguzi umeahirishwa hadi mwezi Machi mwaka 2019 wamepiga kura hewa ili kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) kuahirisha uchaguzi katika maeneo matatu ya nchi hiyo Beni, Butembo na Yumbi, Magharibi mwa nchi.

Mashirika ya vijana na wakazi wa Beni wametenga vituo kadhaa vya kupiga kura na wakazi wa mji huo waliitikia wito wa mashirika hayo kuja kupiga kura.

Mapema wiki hii, Tume ya Uchaguzi (CENI) katika taarifa yake imesema, sababu ya uchaguzi huo kuahirishwa hadi mwezi Machi mwaka 2019, ni kwa sababu ya changamoto za kiusalama katika maeneo hayo ambayo yameendelea kushuhudia mashambulizi ya makundi ya waasi.

Wapiga kura milioni 40 wamepiga kura kumchagua rais wao mpya atayemrithi rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila Kabange.Tume ya Uchaguzi inasema, mshindi atatangazwa tarehe 15 na kuapishwa tarehe 18 mwezi Januari.

Hakuna duru ya pili ya Uchaguzi nchini DRC, anayeshinda atatangazwa na Tume hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.