Pata taarifa kuu
DRC-KABILA-SIASA-USALAMA

Kabila aondoka madarakani, DRC yafunua ukurasa mpya

Rais Joseph Kabila, baada ya kuongoza nchi yake kwa miaka 17, anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo katikati ya mwezi Januari mwaka 2019, lakini wengi,wanajiuliza kuhusu nani atakayechukua nafasi yake.

Rais wa DRC, Joseph Kabila, katika sherehe Septemba 2018 Kinshasa.
Rais wa DRC, Joseph Kabila, katika sherehe Septemba 2018 Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombea 21 wanawania urais, lakini ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi.

Shadary anawakilisha muungano wa chama tawala na alichaguliwa na rais Kabila, kumrithi.

Kabla ya kuwania urais, alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani na alifahamika sana kwa kuwa na msimamo mkali wa kuunga mkono maamuzi ya rais Kabila.

Hata hivyo, anakabiliwa na vikwazo kutoka kwa Umoja wa Ulaya, baada ya mwaka 2007 kuamuru vikosi vya usalama kuzima kwa ukatili mkubwa maandamano ya wapinzani jijini Kinshasa na vifo kadhaa.

Martin Fayulu, yeye anawakilisha muungano wa upinzani Lamuka, anaungwa mkono na aliyekuwa Gavana wa Katanga Moise Katumbi Chapwe na makamu wa rais wa zamani Jean Pierre Bemba.

Felix Tshisekedi, mtoto wa mwanasiasa mkongwe marehemu, Etienne Tshisekedi anawania chini ya chama kikuu cha upinzani UDPS, aliamua kuwania baada ya wanasiasa wa upinzani kugawanyika kuhusu mgombea mmoja. Yeye na Vital Kamerhe walijiondoa kwenye muungano wa wanasiasa waliokuwa wamekubaliana kumuunga mkono Bwana Fayulu katika Uchaguzi huu.

Tume ya Uchaguzi inasema, mshindi atatangazwa taerehe 15 na kuapishwa tarehe 18 mwezi Januari.

Hakuna duru ya pili ya uchaguzi nchini DRC, anayeshinda atatangazwa na Tume hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.