Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-MAANDAMANO

Muungano wa upinzani Lamuka watoa wito wa kuandamana dhidi ya hatua ya CENI DRC

Muungano wa upinzani nchini DRC Lamuka unaowakilishwa na mgombea urais Martin Fayulu, umetoa wito wa maandamano na mgomo wa siku nchi nzima kupingwa kuahirishwa kwa uchaguzi katika maeneo ya Beni, Butembo na Yumbi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi, Desemba 20, 2018 Kinshasa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC (CENI) Corneille Nangaa na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi, Desemba 20, 2018 Kinshasa. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi maafisa wa polisi walipambana na waandamanaji mjini Beni na Goma kupinga hatua hiyo ya CENI kuelekea Uchaguzi wa siku ya Jumapili.

Hata hivyo rais wa nchi hiyo Joseph Kabila akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, amefafanua kuhusu sababu za Tume ya Uchaguzi kuahirisha uchaguzi katika maeneo hayo.

Kwa upande wa chama cha upinzani cha UDPS kimesema hawaungi mkono hatua hiyo na wanaitaka CENI kubatilisha uamuzi huo ili kuwapa haki raia wa maeneo hayo kupiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.