Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-CENI-MASHINE

Wapinzani nchini DRC, wahofia kura kuibiwa kupitia laini za simu

Wagombea wa upinzani wanaowania urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaendelea kuhofia kuwa laini za simu zitakazotumiwa katika mashine za kupigia kura, huenda zikatumiwa na Tume ya Uchaguzi kusababisha udanganyifu wakati wa kuhesabu kura za urais baada ya Uchaguzi siku ya Jumapili. 

Martin Fayulu mgombea wa urais kupitia muungano wa upinzani Lamuka, akizungumza na Wanahabari Desemba 25 2018 jijini Kinshasa
Martin Fayulu mgombea wa urais kupitia muungano wa upinzani Lamuka, akizungumza na Wanahabari Desemba 25 2018 jijini Kinshasa REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na mgombea wa muungano wa upinzani Lamuka, Martin Fayulu, amesema laini hizo haziwezi kuaminika licha ya hakikisho la mara kwa mara kutoka kwa Tume ya Uchaguzi huo, kuwa, kura zote zitahesabiwa kwa mkono.

Mashine za kupigia kura zimeendelea kuzua hali ya sintofahamu na kutoaminiana kati ya wanasiasa wa upinzani na Tume ya Uchaguzi, licha ya hakikisho kutoka kwa Tume hiyo kuwa zoezi hilo litakuwa huru na haki.

Wagombea hao wanataka, Tume ya Uchaguzi kuziandikia barua kampuni za simu ili zifunge laini hizo ambazo CENI imesema zimepachikwa ndani ya mashine hizo za kupigia kura.

Reubens Mikindo, Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha UDPS, ambaye mgombea wake ni Fleix Tshisekedi, ameiambia RFI Kiswahi kuwa, wanakwenda kwenye uchaguzi huu, lakini hawaiamini Tume ya Uchaguzi na matumizi ya mashine hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.