Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Waandamanaji thelathini na saba wauawa Sudan

Waandamanaji thelathini na saba "wameuawa kwa kupigwa risasi" na vikosi vya usalama katika kipindi cha siku tano za maandamano dhidi ya hali ngumu ya maisha nchini Sudan, kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Amnesty International.

Maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta. Khartoum, Septemba 25, 2013.
Maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta. Khartoum, Septemba 25, 2013. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya watu wenye hasira yaliyoikumba miji kadhaa ya Sudan, yalizuka Desemba 19 kufuatia uamuzi wa serikali wa kupandisha mara tatu bei ya mkate katika nchi hiyo inayokabiliwa na mdororo wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa viongozi na mashahidi, maandamano hayo yaliuawa watu wasiopungua nane na sita katika mji wa Al-Gadaref, mashariki mwa nchi na wawili huko Atbara, pia mashariki mwa nchi - wakati wa makabiliano na kikosi cha kuzima ghasia.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Sadek al-Mahdi, amebaini kwamba watu 22 ndio waliuawa, akilaani "ukandamizaji uliofanywa na vikosi vya usalama kwa amri ya serikali."

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu usiku, Amnesty International inaripoti kuwa "waandamanaji 37 walipigwa risasi na maafisa wa usalama wakati wa siku tano za maandamano ya kupinga serikali."

"Ukweli kwamba vikosi vya usalama vinatumia nguvu ya kupita kiasi kwa kutekeleza ukatili dhidi ya waandamanaji wasio na silaha ni hali ambayo inatia wasiwasi sana," amesema Sarah Jackson, naibu mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya Afrika Mashariki, Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika.

Amnesty International limetoa wito kwa serikali "kukomesha matumizi hayo ya mauaji ya kikatili na kuzuia kumwagika damu".

Siku ya Jumatatu Rais wa Sudan Omar al-Bashir aliapa kufanya "marekebisho halisi" baada ya siku za maandamano ya mauti huku kiongozi wa upinzani akitaka jumuiya ya kimataifa kufanya uchunguzi kufuatia vifo vya waandamanaji 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.