Nangaa, ameimbia Televisheni ya Ufaransa, TV5 Monde kuwa, mashine hizo zitasaidia kupeperusha matokeo hayo kutoka vituo vya kupigia kura, baada ya kura kuhesabiwa kutoka kwenye masanduku ya kupigia kura.
“Hata bila kuwepo kwa mashine za kupigia kura, matokeo yalipeperushwa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2006 na 2011, kwa maafisa kupiga simu kutoka kwa vituo vya kupigia kura,” amesema Nangaa.
Mbali na wanasiasa wa upinzani, Kanisa Katoliki, wanaharakati na Marekani, wameonya kuhusu matumizi ta mashine hizo ambazo wamesema, zinaweza kutumiwa kuiba kura.
Hata hivyo, chama tawala PPRD kimesema matumizi ya mashine hizi ndio njia pekee na salama, kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unakuwa huru na haki.