Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-USALAMA

Lucha yapinga hatua ya kuahirisha uchaguzi katika maeneo matatu DRC

Shirika la haki za binadamu nchini DRC, Lucha limetangaza kwamba linatarajia kuanza mfululizo wa maandamano ya kupinga hatua ya Tume ya uchaguzi Ceni ya gusogeza mbele uchaguzi katika maeneo matatu nchini humo kiwa ni pamoja na Butembo na Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Wanaharakati wa Lucha katika maandamano ya mazishi ya mwanaharakati wa Demokrasia Luc Nkulula Juni 14, 2018 Goma.
Wanaharakati wa Lucha katika maandamano ya mazishi ya mwanaharakati wa Demokrasia Luc Nkulula Juni 14, 2018 Goma. Alain WANDIMOYI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Eneo la tatu ni Yumbi lilopo magharibi mwa nchi ambapo watu zaidi ya 100 wameliuawa wiki iliyopita katika makabiliano ya kikabila.

Butembo na Beni ni ngome za upinzani ambazo zimekuwa zikipambana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola tangu mwezi Agosti mwaka huu.

Katika taarifa yake, tume ya uchaguzi (CENI) imesema hatua hiyo inatokana na kusambaa kwa Ebola katika maeneo ya Beni na Butembo pamoja na kudorora kwa amani katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (CENI) matokeo ya uchaguzi wa maeneo hayo matatu hayataathiri mbio za urais kwa sababu mshindi atatangazwa Januari 15 na kuapishwa Januari 18.

Tayari hatua hiyo imeanza kuibua upinzani mkubwa kutoka upinzani. Martin Fayulu, mmoja kati ya wagombea wakuu wa upinzani, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba anapinga hatua hiyo.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana ili uchaguzi ufanyike wanatarajiwa kukutana ili kutoa tamko la pamoja kutokana na hatua hiyo mpya.

Uchaguzi ambao ulitakaiwa kupigwa siku ya Jumapili Desemba 23 mwaka huu .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.