Pata taarifa kuu
CHAD-UFARANSA-USHIRIKIANO

Chad: Macron akaribisha ushirikiano wa kijeshi na aahadi msaada wa kifedha

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliondoka Jumapili usiku katoka mji mkuu wa Chad Ndjamena ambako aliwasili siku ya Jumamosi usiku ili kushiriki chakula cha Krismasi na askari wa kikosi cha Barkhane wanaopiga kambi katika mji mkuu wa Chad.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake Idriss Déby (kulia) katika mkutano wao na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, Desemba 23.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) na mwenzake Idriss Déby (kulia) katika mkutano wao na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, Desemba 23. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa ziara yake ya sita katika eneo la Sahel - lakini ya kwanza nchini Chad - Rais wa Ufaransa, ambaye alipokelewa kwa chakula cha mchana na mwenzake Idriss Deby, amesisitiza kwa muda mrefu juu ya ubora wa uhusiano wa Ufaransa na Chad.

Ingawa kwa ziara yake nchini Chad ilidumu saa 24 tu, Emmanuel Macron alitumia muda huo kwa kufanya mahojiano mawili yaliyochukuwa muda mrefu na mwenzake Idriss Déby, mshirika mkubwa wa rais wa Ufaransa.

Rais Macron amepongza mara kadhaa ushirikiano wa majeshi ya Chad kwa askari wa kikosi cha Ufaransa cha Barkhane katika kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel.

Rais wa Ufaransa alikaribisha ushirikiano mzuri katika nyanja ya usalama kati ya Paris na Ndjamena, "ushirikiano wa miaka mingi," rais wa Ufaransa amesema.

Rais Emmanuel Macron amebaini pia kwamba Ufaransa itaendelea kutoa msaada wake wa kiuchumi kwa Tchad, nchi ambayo inakabiliwa na mgogoro mkubwa.

Boko Haram na G5 Sahel

Baada ya kukiri changamoto nyingi za usalama zinazoikabili Chad, Emmanuel Macron amekubali kutoa msaada kwa Rais Déby. "Rais ametaja umuhimu wa usalama katika Ziwa Tchad, na uwepo wa Boko Haram. Kuhusu suala hili, tuna wasiwasi mkubwa. Kwa hiyo nataka kusema tu kuhusu ahadi za Ufaransa kwa kuunga mkono na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika nyanja zote. Tutakuepo kwa kuharakisha msaada wa Umoja wa Ulaya: euro milioni 55 zinapaswa kutolewa. itafanya kilio chini ya uwezo wake ili fedha hizo zitolewe haraka, " amesema Rais Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.