Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-CENI-IFOKU-MWANAMKE

Marie-Josée Ifoku, mgombea pekee mwanamke anayewania urais nchini DRC

Baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuahirishwa hadi Desemba 30, wananchi wa taifa hilo la Afrika ya Kati, wana imani kuwa, Tume ya Uchaguzi CENI, haitabadilisha tena tarehe hiyo.

Mgombea urais nchini DRC Marie-Josée Ifoku
Mgombea urais nchini DRC Marie-Josée Ifoku www.africanstand.com
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la uchaguzi kuahirishwa liliwakasirisha na kuwavunja moyo wapiga kura waliokuwa wamejiandaa kumchagua rais mpya tarehe 23, baada ya miaka 17 ya rais Joseph Kabila.

Tume ya Uchaguzi ilieleza kuwa ilichukua uamuzi huo kwa sababu ya kuteketea kwa vifaa vya kupigia kura katika jengo la CENI jijini Kinshasa, na walihitaji wiki moja zaidi ili kupata vifaa vipya.

Kuelekea Uchaguzi huo, wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, kati ya wagonbea 20, ushindani unatarajiwa kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu anayewakilisha muungano wa upinzani Lamuka, na Felix Tshisekedi kutoka chama cha UDPS.

Kati ya wagombea hao, mwanamke ni mmoja Marie-Josée Ifoku ambaye naye anasema ana matumaini kuchaguliwa kuwa rais mpya wa DRC.

Ifoku mwenye umri wa miaka 53, alizaliwa jijini Kinshasa katika familia ya kitajiri ya mwanadiplomasia, na maisha mengi aliishi nje ya nchi hasa nchini Canada, alikohudumu mzazi wake.

Mgombea urais nchini DRC Marie-Josée Ifoku
Mgombea urais nchini DRC Marie-Josée Ifoku twitter.com/PR_Pau

Mgombea huyu ambaye pia ni Mfanyibiashara, hasa ya uuzaji wa magari anaamini kuwa DRC inahitaji rais mwanamke kwa sababu ni waaminifu.

“Wanawake wanapofanya kazi katika idara za serikali, wanakuwa waaminifu sana, hawaibi fedha za umma,” amemwambia Mwandishi wetu Freddy Tendilonge akiwa jijini Kinshasa.

Mbali na baishara, yeye ni Mhubiri wa Kanisa la Marie-Josée Ifoku, na anasema kuwa alipata maono kutoka kwa Mungu, ili awe rais kwa lengo la kuibadilisha nchi yake.

Alianza siasa mwaka 2015, akawania ubinge lakini pia akachaguliwa kuwa Naibu Gavana wa jimbo la Tshuapa, lakini mwaka mmoja baadaye akajiuzulu na kuanza harakati za kuwania urais, akisisitiza kuwa Uchaguzi ni lazima ufanyike mwaka 2016.

“Natamani wananchi wa DRC, waishi maisha mazuri, wamiliki mali na kumpa nafasi Mwanamke fursa ya kuongoza, kwa mara ya kwanza, baada ya uhuru wetu,” ameongeza.

Alikuwa amepanga kuachana na mbio za kuwa rais, iwapo upinzani ungempata mgombea mmoja anayekubaliwa na kila mmoja, lakini aliamua kuendelea, baada ya wanasiasa kushindwa kuelewana.

Imemtaka rais wa Tume ya Uchaguzi CENI Cornell Naanga kujiuzulu kwa kushindwa kuandaa uchaguzi wa Desemba 23 2018.

Ripoti ya mwandishi wetu Freddy Tendilonge, akiwa jijini Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.