Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UCHAGUZI

Kusogezwa mbele uchaguzi DRC kwapokelewa kwa shingo upande

Viongozi wa upinzani nchini DR Congo wamelaani hatua ya CENI kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi uliokuwa ufanyike Desemba 23 wakati huu ajali ya ndege iliyokuwa na vifaa vya uchaguzi vya CENI ikiongezea changamoto kwa zoezi hilo kufanyika kama ilivyopangwa.

Raisi wa Tume ya uchaguzi DRC Céni, Corneille Nangaa,akizungumza na vyombo vya habari jijini Kinshasa 20 décembre 2018.
Raisi wa Tume ya uchaguzi DRC Céni, Corneille Nangaa,akizungumza na vyombo vya habari jijini Kinshasa 20 décembre 2018. ISSOUF SANOGO, Luis TATO / AFP
Matangazo ya kibiashara

CENI imeeleza ndege aina ya Antonov 26 ya Urusi iliyoandaliwa na tume ya uchaguzi kutoa vifaa vya uchaguzi ilianguka Alhamisi karibu na jiji la Kinshasa.

Ndege hiyo, iliyoendeshwa na kampuni ya Gomair, ilipata ajali ilipokaribia kutua katika uwanja wa ndege wa jiji hilo baada ya kutoka mji wa Tshikapa ambako ilisambaza karatasi za kutolea matokeo ya uchaguzi.

Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo inatofautiana ambapo ofisi ya ubalozi wa Moscow imenukuliwa ikitaja watu watatu raia wa Urusi wamefariki dunia.

Ajali hiyo inakuja wakati mapema alhamisi tume ya uchaguzi CENI ikitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi hadi jumapili ijayo Decemba 30 kufuatia uharibifu wa vifaa vya uchaguzi katika ghala lililoteketea kwa moto kinshasa juma lililopita hatua iliyopingwa na baadhi ya wagombea lakini raia kuipokea kwa shingo upande.

Uchaguzi wa DRC umekuwa ukisogezwa mbele kwa zaidi ya miaka miwili sasa, huku rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila akishutumiwa kwa kutoa visingizio kadhaa vya kuahirisha uchaguzi ili aendelee kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.