Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-GRACE MUGABE-HAKI

Grace Mugabe atafutwa na vyombo vya sheria vya Afrika Kusini

Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, kwa madai ya kumpiga mlimbwende Gabriella Engel jijini Johannerburg mwaka uliopita.

Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe.
Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe. Zanu-PF/handout
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanamtafuta Bi.Mugabe, baada ya Mahakama kuondoa kinga ya kufunguliwa kwake mashtaka.

Gabriella ambaye anadai alijeruhiwa na Bi. Mugabe alikuwa na watoto wa kiume wa Mugabe, Robert na Chatunga, wakati aliposhambuliwa.

Gabriella Engels alimshutumu Grace Mugabe kwa kumpiga katika chumba cha hoteli mjini Johannesburg.

Serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bibi Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.