Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Afisa wa zamani wa Al Shabab atengwa katika siasa Somalia

media Serikali ya Mogadishu imemzuia Mukhtar Robow, mmoja wa waanzilishi wa Al Shabab, kuwania uongozi katika Jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia. Hali hii ilisababisha tume ya uchaguzi katika eneo hiulo kujiuzulu. REUTERS/Feisal Omar

Serikali ya Somalia, inasema msemaji wa zamani wa kundi la Al Shabab Mukhtar Robow ameondolewa katika orodha ya wale wanaowania uongozi wa majimbo nchini humo.

Siku ya Jumapili, kutakuwa na Uchaguzi wa majimbo na Robow aliyekamatwa wiki hii, alikuwa ametangaza kuwa angewania urais wa jimbo la Kusini Magharibi.

Wakati wa kukamatwa kwake katika eneo la Baidoa, watu wengine 11 walipoteza maisha.

Wakati huo huo Jeshi la Marekani limesema limewaua wapiganaji 62 wa kundi la kiislamu la Al Shabab kwa mashambulizi sita ya anga nchini Somalia.

Haya ni mashambulizi makubwa kuwahi kutokea tangu mwezi Novemba mwaka 2017, pale Marekani ilipowaua wanamgambo 100.

Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya anga tangu Rais wa Marekani Donald Trump aingie madarakani mwezi Januari mwaka 2017.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana