Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Serikali mpya ya Bolivia yamtambua Guaido kama rais wa Venezuela (waziri)
Afrika

Rais wa Sudan akutana kwa mazungumzo na rais wa Syria

media Picha iliyotolewa na shirika la Habari la Sana Desemba 16, 2018 ikionyesha Rais wa Syria Bashar al-Assad (kulia) akimpokea mwenzake wa Sudan Omar al-Bashir (kushoto) kwenye uwanja wa ndege wa Damascus. © AFP

Rais wa Sudan Omar al-Bashir amefanya ziara fupi Damascus na kukutana na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad. Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Omar al-Bashir nchini Syria tangu kuzuka kwa maandamano makubwa nchini humo mwaka 2011.

Bashir amefanya ziara "muhimu" nchini Syria, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Sudan alisema katika uwanja wa ndege wa Khartoum Jumapili jioni, baada ya ndege ya rais kutua.

Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Syria, Assad amekaribisha ziara hiyo, ambayo amesema "itachangia kuanza tena kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kama ulivyokuwa kabla ya vita.

Rais Bashir amesema kuwa "Syria, nchi iliyo katika makabiliano na Israeli, haipaswi kuwa dhaifu," kwa mujibu wa shirika la Habari la Sana.

Pia amesema ana matumaini kuwa "Syria itarejea haraka katika Jumuiya Kimataifa, mbali na uingiliaji wowote wa kigeni katika masuala yake," chanzo hicho kimesema.

Wakati wa mazungumzo yao, Bashir na Assad wameomba kuanzishwa "mbinu mpya katika uhusiano kati ya nchi za Kiarabu zenye msingi wa kuheshimu uhuru wa nchi na kutoingilia kati katika mambo yao ya ndani," kwa mujibu wa shirika la Habari la Sana.

Syria imetengwa katika Jumuiya ya nchi za Kiarabu tangu kusimamishwa kwenye jumuiya hiyo mwezi Novemba 2011, miezi michache tu baada ya kuzuka kwa maandamano makubwa nchini humo.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, mawaziri kadhaa wa mambo ya kigeni wa nchi za Kirabu walifanya ziara katika mji wa Syria, Damascus, kwa mazungumzo rasmi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana