Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

UN yasikitishwa na vurugu za uchaguzi nchini DRC

media Wafuasi wa mgombea urais kwa tiketi ya upinzani DRC Martin Fayulu wakiimba wakati wa kimsubiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'djili Kinshasa, tarehe 21 Novemba 2018. © REUTERS

Kampeni za Uchaguzi zinaendelea nchini DRC mwishoni mwa juma hili, huku wagombea wakiendelea kuwashawishi wapiga kura kuwaunga mkono siku ya kupiga kura tarehe 23 mwezi huu.

 

Wakati kampeni zikiendelea Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imelaani vikali kulengwa kwa wagombea urais kupitia vyama vya upinzani na wafuasi wao.

Mkuu wa Tume hiyo Michelle Bachelet, amesema anasikitishwa sana na mauaji yanayotokea hasa katika mikutano ya wagombea wa upinzani na hadi sasa watu sita wamepoteza maisha.

Mataifa ya Marekani, Canada, Uingereza na Uswizi kupitia mabalozi wao jijini Kinshasa, nao pia wameshtumu mauaji haya ya kisiasa.

Muungano wa nchi za Kusini kwa Afrika SADC, umetoa wito wa utulivu kipindi hiki cha kampeni.

Martin Fayulu, wiki hii akiwa mjini Goma, alisema anasumbuliwa na maafisa wa serikali wanaojaribu kumzuia kufika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kutafuta kura.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana