Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika
DRC

CENI-DRC: Asilimia 80 ya vifaa vya uchaguzi vimeteketea kwa moto

media Wanasiasa kutoka pande zote, wametupiana lawama kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuhusika katika njama za kutaka kuharibu uchaguzi wa Desemba 23 ambapo kuungua kwa mashine za kupigia kura kunazidisha zaidi joto la kisiasa. RFI

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya vifaa vya uchaguzi vilivyokuwa vitumike Desemba 23 jijini Kinshasa, vimeteketea kwa moto baada ya ghala lake moja kuchomwa moto.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI, Corneille Nangaa, amesema vifaa vingi vilivyoungua ni mashine za kielektroniki za kupigia kura zinazopingwa na upinzani.

“Moto huu ni pigo kubwa kwa mji mkuu wa Kinshasa kwa namna ya pekee.CENI imetambua kwamba moto umeteketeza vifaa ambavyo vingetumiwa katika Wilaya 19 za Jiji la Kinshasa lenye Wilaya 24 kwa ujumla. Bila kujali hasara iliyojitokeza, CENI inafanya kila jitihada za kuhakikisha uchaguzi unafanyika kulingana na jinsi kalenda iliyopangwa.”

Hata hivyo Tume ya uchaguzi CENI imesema mashine zilizokuwa zitumike kwenye maeneo mengine zitasafirishwa kutumika jijini Kinshasa.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wameikosoa tume ya uchaguzi kwa kushindwa kudhibiti ulinzi katika ghala hilo huku wakienda mbali zaidi na kudai kuwa ni mpango wa Serikali kutaka kuharibu uchaguzi.

“Ninaishutumu serikali na kuiwajibisha kwa haya yote yaliyotokia, kwa sababu eneo hilo lilipashwa kulindwa sana kuliko mahali pengine hapa nchini, na hii inaonyesha wazi kwamba ni jambo ambalo lilipangwa tangu mwanzo, nasema hivi kwa sababu Serikali hii ilikataa msaada wa Monusco, pia walikataa msaada wa Jumuiya ya kimataifa. Tunaamini wazo hili walikuwa nalo. Na tunatowa wito wapinzani wa kambi nyingine kuachana na lugha yao isiyoeleweka, ” amesema Felix Tschiseked, mgombea wa kiti cha urais kupitia chama kikuu cha upinzani cha UDPS

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, jumla ya vifaa elfu 8 vya kupigia kura viliteketea kati ya mashine elfu 10 na 368 zilizokuwa zitumike Kinshasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana