Pata taarifa kuu
MALI-NIGER-USALAMA

Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi karibu na mpaka wa Niger

Raia kadhaa kutoka jamii ya Tuareg wameuawa kati ya siku ya Jumanne na Jumatano na kundi la watu wenye silaha kaskazini mashariki mwa Mali karibu na mpaka wa Niger, afisa mmoja ameliambia shirika la Habari la AFP.

Doria ya pamoja ya kikosi cha askari wa Ufaransa cha Barkhane jeshi la mali (FAMA, katika mtaa wa Menaka.
Doria ya pamoja ya kikosi cha askari wa Ufaransa cha Barkhane jeshi la mali (FAMA, katika mtaa wa Menaka. GaΓ«lle Laleix/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Kati ya usiku wa Desemba 11 na asubuhi ya ya Desemba 12, watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki zaidi ya ishirini walivamia maeneo kadhaa kusini ya mkoa wa Menaka na kuwauawa kwa risasi raia kutoka jamii ya Idaksahak" (Tuareg)," kundi la Azawad limtebaini, huku likisem akuwa watu zaidi ya 47.

"Baada ya kitendo hicho kihalifu washambuliaji waliondoka na kuelekea kwenye mpaka wa Niger, baada ya kuchoma msitu, limesema kundi hilo la Tuareg linaloshirikiana na jeshi la Ufaransa nchini Mali na jeshi la Mali, ambao mara kwa mara wanakabiliana na mashambulizi ya kundi la IS.

Mamia ya watu, ikiwa ni pamoja na raia wengi, hasa kutoka jamii za Fulani na Tuareg, wamefariki dunia katika kanda hii tangu mwanzo wa mwaka. Viongozi.waliochaguliwa katika eneo la Menaka wamethibitisha shambulio hilo na kusema kuwa watu kati ya Ishini na 40 waliuwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.