Pata taarifa kuu
DRC-CENI-UCHAGUZI

CENI DRC: Vifaa vya uchaguzi vimewasili katika maeneo mbalimbali ya nchi

Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) imetangaza kwamba vifaa vyote vya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na "mashine za kupigia kura", vimewasili katika maeneo yote na miji mbalimbali ya nchi hiyo tangu Jumatano wiki hii.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja ikiwa zimesalia siku kumi na moja kabla ya Uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23.

"Wapiga kura na wanasiasa mbalimbali wanashuhudia matatizo yanayoikabili Tume Huru ta Taifa ya Uchaguzi (CENI) katika kusafirisha vifaa vya uchaguzi," CENI imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Vifaa hivyo ni pamoja na "mashine za kupiga kura, vibanda vya kupigia kura, masanduku ya kura ...", chanzo kutoka CENI kimeliambia shirika la Habari la AFP.

Tume hiyo ya Uchaguzi imesema kuwa imeorodhesha wapiga kura milioni 40 wanaotarajia kushiriki uchaguzi huo katika vituo vya kupigia kura 80,000 ambavyo vitakuwa na 'mashine za kupigia kura" zaidi ya 100,000.

Hata hivyo wanasiasa wa upinzani wanaona kwamba mashine hizo haziaminiki na zitatumiwa kwa kuiba kura.

Mgombea wa upinzani Martin Fayulu anapinga utaratibu huo wa kupiga kura. Mgombea mwengine Felix Tshisekedi yuko tayari kushiriki uchaguzi hata kama kutatumiwa au la "mashine za kupigia kura", lakini wafuasi wake wanasema wako tayari kubaki katika vituo vya kupigia kura hadi dakika ya mwisho.

Mapema wiki hii kampeni za mgombea urais Martin Fayulu ziligubikwa na machafuko. Watu wasiopungua wawili waliuawa katika makabiliano na polisi wakati Martin Fayulu alipowasili Kalemie katika mkoa wa Tanganyika, ngome ya Rais Joseph Kabila.

Siku moja kabla, watu wengine wawili waliuawa katika makabiliano na polisi huko Lubumbashi, kwa mujibu wa mashirika yasio ya kiserikali. Kufuatia hali hiyo Martin Fayulu aliamua kufuta mkutano wake wa hadhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.