Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Serikali mpya ya Bolivia yamtambua Guaido kama rais wa Venezuela (waziri)
Afrika

Watoto wengi waambukizwa virusi vya Ebola DRC

media Kitengo kinachohusika na kuwaondoa wagonjwa wa Ebola katika makazi ya watu, DRC wakati wa mlipuko wa virusi vya Ebola mwaka 2009. Luis Encinas/MSF

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu robo tatu ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni watoto, huku mamia kati yao wakiwa ama ni yatima au kutengwa na familia zao.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO jumla ya watu 300 wameshapoteza maisha tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Agosti mwaka huu huku visa vingi vikiripotiwa kwenye mji wa Beni.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linasema kuwa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kiraia wamebaini watoto zaidi ya 400 ambao wamekuwa yatima au kutengwa na familia zao tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukabiliwa na ugonjwa wa Ebola, ambao kwa mara ya kwanza umeripotiwa nchini humo mwaka 1976.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana