Pata taarifa kuu
CAR-UFARANSA-USHIRIKIANO-USALAMA

Ufaransa yakabidhi silaha za kivita 1,400 kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Serikali ya Ufaransa juma hili imekabidhi bunduki zaidi ya elfu 1,400 aina ya AK-47 kwa vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati vinavyokabiliana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha.

Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.
Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Florence Parly alishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye kambi ya jeshi ya M’Polo iliyoko mjini Bangui.

Msaada huu wa kijeshi ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya Ufaransa iliyoitoa mwezi Novemba jijini Paris, sambamba na euro milioni 24 kama msaada wa kibinadamu.

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepoteza maisha katika mapigano huku wengine zaidi ya laki 7 wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine zaidi ya laki 5 wakiikimbia nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.