Pata taarifa kuu
DRC-EU-VIKWAZO

DRC yashtumu Umoja wa Ulaya kuingilia katika masuala yake ya ndani

Serikali ya DRC imepinga vikali uhalali wa vikwazo vipya vilivyochukuliwa Jumatatu, Desemba 10 na Umoja wa Ulaya dhidi ya maofisa 14 wa nchi hiyo ambao wanashtumiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kukwamisha mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC.
Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC. Junior D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa serikali ya Kinshasa, vikwazo vya Umoja wa Ulaya vinavyomlenga Emmanuel Ramazani Shadary, mgombea wa rais Joseph Kabila katika uchaguzi wa urais, ni jambo "lisilokubalika" kwa sababu Umoja wa Ulaya unaingilia kisiasa katika "mchakato wa uchaguzi".

Umoja wa Ulaya unasema umelazimika kuchukua vikwazo hivyo kama "hatua za kuzuia" kutokea matatizo ya kisiasa". Kwa hiyo vinaweza kufutwa kama kutakuwa na "maendeleo yoyote yanayoonekana", chanzo cha kidiplomasia kimebaini.

Vinginevyo, vikwazo hivyo vinaongezewa muda kila mwaka.

Serikali ya DRC inasema hatua hizo zimechukuliwa kinyume cha sheria, na kushtumu kuwa umoja wa Ulaya haukutoa nafasi kwa maafisa hao kujieleza kuhusiana na madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.