Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-RWANDA-USHIRIKIANO

Afrika Kusini yamuita nyumbani balozi wake Rwanda

Serikali ya Afrika Kusini imemuita nyumbani balozi wake nchini Rwanda kwa mazungumzo baada ya hivi karibu afisa mmoja wa Rwanda kutoa matamshi ya kejeli dhidi ya Waziri wake wa Mambo ya Nje, Lindiwe Sisulu.

Gazeti la Rushyashya lilichapisha habari iliyomkashifu waziri Lindiwe Sisulu kutokana na matamshi yake kumuhusu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa.
Gazeti la Rushyashya lilichapisha habari iliyomkashifu waziri Lindiwe Sisulu kutokana na matamshi yake kumuhusu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa. RODGER BOSCH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kuwa, wakati Serikali ya rais Cyril Ramaphosa ikijaribu kurejesha uhusiano wa kawaida na Kigali, matamshi yanayodaiwa kuwa ya kejeli dhidi ya waziri wake wa mambo ya nje, yamezidisha sintofahamu zaidi.

Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imethibitisha kuitwa nyumbani kwa balozi wa Afrika Kusini lakini haikusema wazi ikiwa kuitwa kwake kuna uhusiano wowote na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Juma moja lililopita gazeti la Rushyashya lilichapisha habari iliyomkashifu waziri Sisulu kutokana na matamshi yake kumuhusu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda jenerali Kayumba Nyamwasa.

Tangu Afrika Kusini isema inachunguza mauaji ya Patrick Karegeya, uhusiano wa nchi hizo mbili umetetereka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.