Pata taarifa kuu
DRC-EU-VIKWAZO

Umoja wa Ulaya waendelea na vikwazo dhidi ya maafisa waandamizi DRC

Umoja wa Ulaya umeongeza muda wa vikwazo kwa maafisa kadhaa nchini DRC hadi Desemba 12, 2019. Hatua hiyo imechukuliwa Jumatatu wiki hii katika kikao cha umoja huo mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC.
Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi kutoka chama tawala cha PPRD nchini DRC. Junior D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ramazani Shadary, aliyeteuliwa mwaka huu kuwakilisha kambi ya Kabila katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 23, alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kati ya mwezi Desemba 2016 na mwezi Februari 2018.

Umoja wa Ulaya unamchukulia kama mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu aliyehusika katika visa vya kukamatwa kwa wapinzani na "ukandamizaji wa kikatili" dhidi ya maandamano yaliyotokea mwezi Januari hadi Februari 2017 mjini Kinshasa, kulingana na hati rasmi ya Umoja wa Ulaya.

Pia kuna suala la "matumizi yasiyo ya kawaida ya nguvu" ikwa kuliangamiza vuguvugu la kidini la Bundu Dia Kongo (BDK) na maandamano mengine huko Kasai, katikati mwa nchi.

Mwezi Mei 2017, jina la Ramazani Shadary lilikuwa miongoni mwa viongozi tisa wa vyombo vya usalama nchini DRC waliyoongezwa kwenye orodha ya viongozi saba ambao tayari wanakabiliwa na vikwazo kufuatia machafuko yaliyotokea mnamo mwezi Septemba 2016.

Vikwazo hivi vinavyowakabili maafisa hao waandamizi drc ni pamoja na kuzuia mali zao na kunyimwa visa ya kuingia katika moja ya nchi mwanachama wa Umoja aw Ulaya.

Waziri wa Habari na Msemaji wa Serikali Lambert Mende, ni miongoni mwa maafisa 14 wanaokabiliwa na vikwazo hivyo vya Umoja aw Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.