Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Brexit: Brussels yataka 'kujenga upya' uhusiano na London baada ya ushindi wa Johnson (Breton)
 • Donald Trump ampongeza Boris Johnson kwa ushindi wake 'mkubwa' katika uchaguzi wa wabunge Uingereza
Afrika

Daraja linalounganisha Kivu Kaskazini na Uganda lavunjika, uchumi matatani Beni

media Mtoto akicheza karibu na daraja lililovunjika kufuatia mafuriko mjini Kampala Mei 8, 2013. (Picha ya inayoashiria tukio lililotokea) © REUTERS

Wafanyabiasaha katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wameelezea masikitiko yao kufuatia kuvunjika kwa daraja linalounganisha mkoa wa Kivu Kaskazini na Uganda. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili.

Daraja la Lubihira katika mji wa Beni unaoendelea kuathirika na ugonjwa wa Ebola na mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la waasi wa Uganda wa ADF lilivunjika.

Mashahidi wanasema daraja hilo lilivunjika wakati lori kubwa aina ya Actros lilikuwa likipita likitokea nchini Uganda. Taarifa hii imethibitishwa na afisa wa serikali katika eneo hilo, Donat Kibwana, akiliambia shirika la Habari la AFP.

"Kwa sasa, tunajaribu kuangalia jinsi ya kuokoa hali kwa kusubiri ukarabati. Vinginevyo mkoa wote kuna hatari ukabiliwe na baa la njaa kwa sababu daraja hili lilikuwa linaounganisha eneo la Mashariki mwa DRC na Uganda na Tanzania," Bw Kibwana ameongeza.

"Eneo hili la mpakani ni muhimu sana kwetu na kwa DRC kwa ujumla. Bidhaa nyingi mahitajio kwa raia wa mkoa wa Kivu Kaskazini hutoka Uganda na huingia nchini hapa kupitia daraja hili," amesema Naibu kiongozi wa shirika la wafanyabiashara la FEC, Cléophace Paluku.

Mwezi Januari 2017, kuvunjika kwa daraja la Semuliki linalounganisha DRC na Uganda kulisababisha bei za bidhaa mahitajio kupanda mara dufu katika mji wa Beni, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini DRC.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana