Afisa huyo wa jeshi la DRC alikuwa anashutumiwa tangu Mei 2017 na Umoja wa Mataifa kuhusika katika mauaji ya wataalamu wake wawili Michael Sharp na Zaida Catalan huko Kasaï ya Kati, bila hata hivyo kuwa na wasiwasi na mahakama ya kijeshi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya nyaraka za siri za Umoja wa Mataifa "Congo Files" kuchunguzwa wiki iliyopita na vyombo vya habari vitano vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na RFI.
Habari hii, kama habari nyingine, ilikuwa imefichwa na Sekretarieti kuu ya Umoja wa Mataifa katika Baraza la Usalama la umoja huo.
Kanali Jean De Dieu Mambweni wakati huu ni mshtumiwa rasmi anayezuiliwa, lakini bado hakuna mashitaka yoyote yanayomkabili.
Jean De Dieu Mambweni awali alikamatwa Novemba 26, lakini aliachiliwa mara moja. Hata hivyo, mmoja wa watuhumiwa wakuu, kiongozi wa kundi la wanamgambo na muuaji, Vincent Manga, alihakikishia wakati kesi yao ikisikilizwa kwamba Kanali Mambweni aliwapa silaha.
Mahakama ya kijeshi ya DRC imetangaza kwamba waranti wa kumkamata Kanali Mambweni imetolewa. Kanali Mambweni mwenyewe amethibitisha hali hiyo kwa simu aliompigia mwanasheria wake.
Jean De Dieu Mambweni hajapatikana na hatia, uchunguzi unaendelea, mahakama ya kijeshi imeongeza.