Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mazungumzo kuhusu Sahara ya Magharibi yaanza Geneva

media Jengo la Mataifa ya Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi. RFI/Paulina Zidi

Mazungumzo kuhusu Sahara ya Magharibi yameanza tangu Jumatano wiki hii baada ya kusitishwa kwa miaka sita. Mazungumzo hayo yanafanyika huko Geneva, nchini Uswisi.

Umoja wa Mataifa unakutana tangu Jumatano wiki hii mjini Geneva, nchini Uswisi kujadili hali ya Sahara ya Magharibi. Tangu kuondoka kwa Uhispania, iliyoitawala nchi hiyo katika enzi za ukoloni mnamo miaka ya 1976, eneo hilo linadhibitiwa 80% na Morocco wakati kundi la Polisario Front linaendelea kuomba uhuru wa eneo hilo.

Mazungumzo, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, yamesimama tangu mwaka 2012. Kutokana na hali hiyo Horst Kohler, Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hili, ameamua kufufua mazungumzo kwa kualika wadau wote mjini Geneva, akiwa na matumaini ya kufikia suluhu ya mgogoro huo wa zamani wa zaidi ya miaka 40.

Wadau wanaokutana kwa muda wa siku mbili huko Geneva hawajakutana tangu mwaka 2012 ili kujadili suala la Sahara ya Magharibi. Eneo ambalo hatima yake imekubwa na kiza kwa miaka kadhaa.

Kwa muda mrefu Sahara Magharibi ilikuwa koloni ya Uhispania. Mnamo mwaka 1975, makubaliano yaliyotiliwa saini mjini Madrid yalimaliza utawala huo wa ukoloni na kugawanya eneo hilo mara mbili. Eneo la kusini mwa Sahara Magharibi lilipewa Mauritania, ambayo ilirejesha sehemu hiyo miaka sita baadaye, wakati eneo la kaskazini na katikati lilichukuliwa na Morocco.

Makubaliano yalitiloiwa saini siku chache baada ya maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Mfalme Hassan II wakati zaidi ya raia 350,000 wa Morocco walizuru eneo hilo. Tangu wakati huo, hali ya mvutano iliibuka kati ya utawala wa Hassan II na kundi la waasi la Polisario Front.

Polisario Front inaomba uhuru wa Sahara ya Magharibi.

Mnamo mwaka 1976, Polisario Front ilitangaza eneo hilo kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sahrawi (SADR). Mwaka 1984, ilijiunga na Umoja wa Afrika (ambayo ilikuwa bado ikiitwa OAU) na Morocco kuamua kujiondoa kwenye taasisi hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana