Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-USALAMA

Wagombea katika uchaguzi wa urais waendelea kunadi sera zao DRC

Kampeni za uchaguzi mkuu zimeendelea kupambana nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, zikiwa zimesalia siku kumi na nane, wananchi wa taifa hilo wapige kura.

Tume ya uchaguzi DRC (CENI) yaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Desemba 23.
Tume ya uchaguzi DRC (CENI) yaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Desemba 23. AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa kiti cha urais katika kambi yaupinzani Felix Tshisekedi akiandamana na Vital Kamerhe wamekuwa mjini Goma, huku Mgombea kwa tiketi ya chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary amekuwa Gbadolite kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Wakiwa mjini Goma mashariki mwa Nchi hiyo siku ya Jumanne Vital Kamerhe ambaye hivi karibuni aliungana na Felix Tshisekedi waliahidi kuwa muungano wao unalenga kuwanufaisha wananchi wa nchi hiyo, huku wakiahidi kuimarisha usalama wa eneo hilo linalokumbwa na machafuko.

Haya yanajiri wakati Felix alidhihirisha nia yake ya kulijenga taifa hilo, huku akisema yaliyopita yamepita ni muda wa kuganga yajayo.

Kwa upande wake mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadari akiwa mjini Gbadolite kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, ambako alilakiwa na maelfu ya wafuasi wa muungano wa vyama tawala, Shadary aliahidi kuwa ataboresha maisha ya wananchi wa eneo hilo ambao alisema wamesahaulika tangu enzi za marehemu Mobutu.

Henry Mova Sakanyi, mmoja wa wanasiasa mashuhuri upande wa serikali amesema wana imani Shadary atashinda.

Katika hatua nyingine wakati kampeni hizi zikiendelea, wagombea wakuu wameanza kuwavutia wagombea wadogo wasio na umaarufu, ambapo Triphon Kinkey Mulumba kutoka upande wa vyama madarakani ameamua kujiunga na felix Tshisekedi.

Wakati mwanasiasa mwengine Jean Philbert Mabaya wa chama cha Kisiasa Arc en Ciel yeye ameamua kumuunga mkono Martin Fayulu.

Uchaguzi wa DRC umepangwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu wa desemba huko DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.