Rais wa Gabon aonekana hadharani baada ya kulazwa hospitali kwa miezi kadhaa
Rais wa Gabon Ali Bongo, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza, akiwa nchini Morocco, baada ya kuwasilia nchini humo siku chache zilizopita akitokea nchini Saudi Arabia alikokuwa amelazwa.
Imechapishwa:
Rais Bongo, anapata mapumziko ya baada ya matibabu kabla ya kurejea jijini Libireville, na ameonekana kwa mara ya kwanza, akiwa na Mfalme wa nchi hiyo Mohammed VI aliyeenda kumtembelea.
Ugonjwa unaosumbua, haujawekwa wazi lakini, inaaminika kuwa alipata kiharusi mwishoni mwa mwezi Oktoba, wakati alipokuwa amekwenda nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kimataifa.
Mnamo Novemba 11, msemaji wa ikulu Ike Ngouoni aliwaambia waandishi wa habari kuwa rais Ali Bongo atakuwa mwenye afya nzuri katika siku za hivi karibuni.
Vyombo vya habari nchini Gabon vilikuwa vikifahamisha kuwa huenda rais Ali Bongo akapelekwa mjini Paris au London.
Ali Bongo ni mtoto wa aliekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Omar Bongo ambae aliongoza taifa hilo tangu mwaka 1967 hadi alipofariki Juni 8 mwaka 2009.