Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

kumi nane wauawa katika mapigano kati ya jeshi na waasi nchini DR Congo

media Walinda amani wa Monusco kutoka Pakistani wakipiga doria katika mitaa ya Uvira, wilayani Fizi. MONUSCO/Force

Ikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hali ya usalama inaendelea kudoroara. Askari wanne na waasi 14 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wanaoongozwa na afisa wa zamani aliyeasi, vyanzo vya kijeshi vimesema.

Jumatatu asubuhi, askari na waasi wawili waliuawa katika mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Yakutumba, jina la afisa wa zamani aliyeasi William Amuri Yakutumba, aliyeingia msituni na kutangaza vita dhidi ya Rais Joseph Kabila.

Mapigano yalitokea katika eneo la Fizi, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC.

Wanamgambo hao wanashirikia na waasi wa nchi jirani ya Burundi wa National Liberation Front (FNL), kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika eneo hilo ambvyo vimehojiwa na shirika la Habari la AFP.

"Waasi wamepoteza wapiganaji 12, Kamanda Alida naibu wa Yakutumba ni miongoni mwa waliouawa", amesema msemaji wa jeshi katika eneo hilo, Kapteni Dieudonne Kasereka.

"Askari watatu wamefariki dunia na silaha zao kupotea baada ya kupelekwa na mto," ameongeza Bw Kasereka akiliambia shirika la Habari la AFP.

Mwezi Septemba 2017, kundi la waasi la Yakutumba lilitishia kuendesha mashambulizi moja ya miji mikubwa ya Kivu Kusini, Uvira, wenye bandari kubwa katika ziwa Tanganyika, kilomita 15 na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kiliingilia kati na kutumia helikopta zake na kufalu kuwarejesha nyuma waasi hao.

Mwezi Februari mwaka huu, jeshi la DRC lilisema "liliangamiza" kund la waasi wa Yakutumba wakati mashambulizi dhidi ya ngome zake.

Fizi, eneo lenye utajiri wa madini lilikuwa ngome ya waasi wa Laurent-Désiré Kabila, baba wa rais wa sasa wa DRC, akiongoza waasi wa AFDL, ambao walimtimuwa madarakani Marshal Mobutu Sese Seko na kuchukuwa uongozi wa nchi mnamo mwezi Mei 1997.

Makundi zaidi ya mia moja ya watu wenye silaha yanasadikiwa kuendesha harakati zao mashariki mwa DRC. Uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika Desemba 23 kwa kumchagua mrithi wa Rais Joseph Kabila Kabange na kuwachagua wabunge.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana