Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-ULINZI-USHIRIKIANO

Idadi ya askari wa Marekani yadaiwa kuwa kubwa Afrika

Gazeti la Marekani linalochapisha habari zake mtandaoni The Intercept limechapisha taarifa kuhusu uwepo wa kiasi kikubwa cha wanajeshi wa Marekani barani Afrika.

Ndege ya jeshi la Marekani ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Port-au-Prince.
Ndege ya jeshi la Marekani ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Port-au-Prince. AFP PHOTO / THOMAS COEX
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inaonyesha uwepo mkubwa zaidi wa wanajeshi kuliko ilivyowasilishwa na jeshi la Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Marekani, wanajeshi wa Marekani wapo katika maeneo mbalimbali barani Afrika kwa ajili ya kupamabana na ugaidi wakati huu vituo 34 vimeorodheshwa.

Inaelezwa kwamba idadi ya wanajeshi 7000 wa Marekani wapo barani Afrika wakati huu ukishukiwa kuwa idadi hiyo huenda ni kubwa zaidi ya ile ilivyowasilishwa na Pentagon.

Waziri wa zamani wa Marekani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Jeff Hawkins amesema Marekani inavutiwa na Afrika katika sekta ya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.