Pata taarifa kuu
ULAYA-AFRIKA-UBAGUZI

Ripoti: Watu wenye asili ya Afrika wanabaguliwa barani Ulaya

Ripoti iliyotolewa na taasisi ya Haki za msingi za Umoja wa Ulaya, inaeleza kuwa watu wenye asili ya Afrika wanaoishi barani Ulaya, wanaendelea kubaguliwa na kuchukiwa barani Ulaya.

Ramani ya bara la Afrika na Ulaya
Ramani ya bara la Afrika na Ulaya map
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inaendelea kushuhudiwa katika katika mataifa 12 ya bara hilo.

Kati ya mwaka 2015-2016 watu karibu 6,000 wenye asili ya Afrika walibaguliwa dhidi ya kupata haki za msingi, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Umoja wa Ulaya.

Asilimia 30 ya watu hao wanasema wanabaguliwa kwa misingi ya rangi yai nyeusi, huku asilimia tano wakishambuliwa kwa mujibu wa ripoti hii.

Idadi kubwa ya watu wanaosema wanaendelea kuishi kwa mazingira magumu wapo nchini Finland.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya Finland, kila mmoja anastahili kuhudumiwa kwa usawa bila kujali asili yake au hata jinsia yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.