Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Rajoelina na Ravalomanana kuchuana katika duru ya pili ya uchaguzi Desemba 19

Marais wawili wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina na Marc Ravalomanana, watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi utakao fanyika Desemba 19 mwaka huu.

Marais wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana (kushoto) na Andry Rajoelina (kulia).
Marais wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana (kushoto) na Andry Rajoelina (kulia). (Photos : AFP & flickr)
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao ndio wameshinda katika duru ya kwana ya uchaguzi uliofanyika Novemba 7, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa Jumatano, Novemba 28 na Mahakama Kuu ya Katiba.

Rais Hery Rajaonarimampianina ambaye alikuwa anawania kuteuliwa kwa mara nyingine kuendelea kuongoza taifa hilo, alipata asilimia 8,84 ya kurakulingana na taarifa ya tume ya uchaguzi.

wagombea 36, ikiwa ni pamoja na marais wa zamani wanne, mawaziri wa zamani watatu, wachungaji, na mwanamuziki mmoja ndio walishiriki uchaguzi huo, hata hivyo baadhi walilalama kwamba uchguzi huo uligubikwa na udanganyifu.

Hivi karibuni waangalizi wa Umoja wa Ulaya walisema kuwa wagombea karibu wote walikiuka sheria za uchaguzi kabla ya uchaguzi wa November 7 lakini wakahitimisha kuwa uchaguzi ulifanyika katika mazingira ya uwazi na haki.

Ravalomanana na mwenzake Rajoelina wote walizuiliwa kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 baada ya shinikizo la kimataifa ili kuepusha kujirudia kwa vurugu zilizoshuhudiwa mwaka 2009.

Ravalomanana na Rajoelina ni maadui wa kisiasa na hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hawa kushinda kupitia njia ya upigaji kura.

Ravalomanana aliongoza taifa hilo kati ya mwaka 2002 hadi 2009 alipopinduliwa na jeshi ambalo lilimuweka madarakani Rajoelina aliyetawala hadi mwaka 2014.

Jaribio la mwanzoni mwa mwaka huu la rais Rajaonarimampianina kutaka kurekebisha sheria za uchaguzi lilishindakana baada ya kutokea maandamano makubwa ya kupinga hatua yake.

Waangalizi wa Umoja wa Afrika wametoa wito kwa wagombea wote kujiepusha na utoaji wa matamshi ambayo huenda yakasababisha vurugu ambapo pia umewataka waheshimu utawala wa sheria.

Nchi ya Madagascar ni moja ya mataifa masikini duniani kwa mujibu wa wa takwimu za benki ya dunia, ambapo watu wanne kati ya watano wanaishi chini ya dola moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.