Pata taarifa kuu
DRC-HAKI-USALAMA

Kesi ya kiongozi wa kundi la wanamgambo Sheka yaanza kusikilizwa Goma

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka, kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo "Nduma Defense of Congo" (NDC), imeanza kusikilizwa Jumanne hii (Novemba 27) mbele ya mahakama ya kijeshi ya mjini Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini DRC.

Kiongozi wa kivita Ntabo Ntaberi Sheka katika mkutano Novemba 2011 (picha ya kumbukumbu).
Kiongozi wa kivita Ntabo Ntaberi Sheka katika mkutano Novemba 2011 (picha ya kumbukumbu). STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Usalama umeimarishwa, huku vikosi vya usalama vikiwekwa pembezoni mwa jengo la mahakama ya kijeshi.

Ntabo Ntaberi Sheka anashtumiwa, kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa kijeshi, makosa kadhaa ambayo anadaiwa aliyatekeleza mnamo mwaka 2013, katika eneo la Walikale, Kaskazini mashariki mwa DRC. Makosa hayo ni pamoja na ubakaji mkubwa wa wanawake zaidi ya mia tatu katika maeneo ya Luvungi, Tweno na Kembe.

Anashtumiwa pia kuua zaidi ya raia wanne huko Chobu, Lubonga, Bunyampuri. Sheka na washtumiwa wenzake wanashtumiwa pia kuchoma moto nyumba zaidi ya mia moja katika eneo moja.

Pia anashutumiwa kupora katika vijiji kadhaa na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Anashtumiwa pia kuwa alisajili watoto wadogo kadhaa katika kundi lake la wanamgambo.

Utumwa wa ngono pia ni miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Bw Sheka. Sheka alikamatwa mara kadhaa na kufaulu kutoroka, lakini mnamo mwezi Julai 2017 alijisalimisha mbele ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), kabla ya kusafirishwa mjini Kinshasa mwezi Agosti mwaka huu.

Mahakama ya kijeshi ambayo inashughulikia kesi yake ni mahakama ya kipekee ambayo imewekwa ili kuzuia uhalifu uliofanywa wakati wa vita katika maeneo ya mapigano yalikuwa yakiendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.